Mwakilishi wasi ya butsotso mashariki mathews nyangweso amewataka wazazi ambao wamenufaika na basari kutembelea afisi yake na kupewa barua za kuwawezesha watoto wao kuwa shuleni huku fedha zikisibiriwa
Akihutubu kwenye mazishi ya mzee Gerald Nasilobe katika kijiji cha Shitoto Nyangweso pia ameelezea mipango ya kukarabati barabara eneo hilo
Msimamizi wa shirika la kijamii la Jisimamie Community Based Organisation Cyrus Akhonya ambaye alihudhuria mazishi hayo amewayaka wakazi kushirikiana kuendeleza elimu ya watoto kupitia kwa mradi wa jisimamie elimu initiative
Wakati huo huo viongozi wa serikali mashinani eneo hilo wakiongozwa na senior Liguru wa Murumba Pandya Mukangai na msimamizi wa serikali ya kaunti kijiji cha Shitoto Edward Oponyo walilalama ongezeko la visa vya wizi na kuwataka wakazi kushirikiana kuukomesha
By Lindah Adhiambo