Familia moja kutoka kijiji cha Mukongolo eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega inakadiria hasara ya maelfu ya pesa baada ya shamba la miwa la ekari moja kuteketea kwa njia ya kutatanisha.

Kulingana na familia hiyo ikiongozwa na Catherine Ashiali inadai kuwa moto huo ulizuka mwendo wa saa kumi za alfajiri usiku wa kuamkia leo kabla ya majirani kuingilia kati na kuuzima moto huo.

Hata hivyo juhudi za wenyeji kuuzima moto huo japo kwa kuvumilia makali yake zilifua dafu huku wakiitaka serikali kuanzisha uchunguzi wa haraka wakisema kwa sasa wanaishi kwa hofu baada ya kisa hicho kilichowaacha wengi vinywa wazi.

By Linnet Mukaitsi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE