Kaimu mwenyekiti wa wakulima wa zao la nyanya katika wadi ya Chesikaki eneo bunge la Mlima Elgon, Patrick Cheptum amewataka wanunuzi wa zao hilo kutumia vipimo vinavyostahili ili kuwawezesha wakulima kunufaika na zao hilo.

Akihutubu baada ya mkutano na wakulima wa zao hilo eneo la Chemondi, Cheptum amesema wakulima kutoka eneo hilo wanapata hasara kubwa kutokana na kuzinduliwa kwa kipimo aina ya mananja na kutoa wito kwa serikali ya kaunti ya Bungoma kuwasaidia kupata dawa za kupambana na magonjwa mbalimbali ya mmea huo.

Naye katibu wa wakulima hao Lenox Kimetit akidokeza kuwa watazidi kuwahamazisha wakulima kando na kuwatambua mawakala halali kisha kuwasajili.

Nao wakulima wakiongozwa na Bonface Ndege wamesema kilimo ndicho kiteka uchumi eneo hilo huku  akielezea changamoto wanazokumbana nazo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE