Maji ni uhai na pia bidhaa muhimu kwa maisha ya viumbe vyote hapa ulimwenguni ambapo hutegemewa pakubwa kwa kunywa na usafi wa kila aina.

Lakini kwa mjibu wa  mwalimu mkuu wa washule ya Eshiamboko Josphat Chimwani anasema kuwa wao hupitia  ugumu  kupata maji kwenye shule hiyo ambapo wakati mwingi hulazimu wanafunzi kusafiri mwendo mrefu kutafuta maji wakati huu wa kiangazi.

Kulingana na chimwani hata wanafunzi wengine hukosa masomo kwa kutafuta maji kama njia moja ya  kuhakikisha wanatimiza masharti ya afya ya kunawa mikono kila  wakati kupunguza maambukizi ya virusi hatari vya corona.

 Kwa sasa mwalimu mkuu huyu anatoa wito kwa wahisani na haswa mbunge wa Lurambi Titus Khamala kuingilia kati na kusaidia kumaliza tatizo hili kabla ya maafa kupatikana kwa kukosa maji safi.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE