Mkaguzi wa serikali kuu Nancy Gachungu azuru kaunti ya Kakamega kuikagua mirandi iliyoanzishwa na serikali hivyo chini ya gavana Oparanya.
Akiwahutubia waandishi wa habari nje ya makao makuu ya afisi za kaunti hiyo baada ya kukutana na mawaziri wa kaunti hiyo pamoja na jopo maalum la wakilishi wadi,Nancy amesema lengo lao kama afisi ni kuhakisha miradi iyoanzishwa na serikali hiyo imekamilika kwa wakati.
Aidha mkaguzi huyo wa serikali kuu ameipongeza serikali ya kaunti ya Kakamega kwa kutoa mahali pa kujenga afisi zao jambo litakalorahisisha utenda kazi wao katika uliokuwa mkoa wa magharibi kwa ujumla.
Miongoni mwa miradi waliyoikagua ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Kakamega, uwanja wa michezo wa Bukhungu miongoni mwa mingine.
Kwa upande wake naibu gavana prof Philip Kutima ambaye amekuwa mwenyeji wa maafisa hao amedokezo kuwa lengo la mkaguzi lilikuwa tu kuangazia miradi inayotekelezwa na serikali ya kaunti ya Kakamega bali si kitu kingine tofauti.