Hali ya huzuni na hofu imetanda katika kijiji cha Imadala eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega baada ya mtoto mmoja wa miaka 14 kufariki huku wengine wanne wa umri wa kati ya miaka 8 na 12 akiwemo wa jirani wakiendelea kutibiwa katika hospitali ya Kakamega na Shamakhubu mmoja akiwa hali mahututi baada ya kula ndizi inadaiwa kuwekwa sumu.
Familia ya watoto hao ikiongozwa na Nifa Lukholo ambaye ni nyanya wa watoto hao anasema kuwa alipika ndizi hiyo na kuenda kwa shughuli zake za boma na alipoiondoa kwenye meko na kuwapa watoto hao , walikula japo walianza kulalama kuumwa na tumbo kabla ya kuanza kuhara na kutapika na kupelekea mmoja wao wa miaka 14 kwa jina Melvin Ikalakala kufariki.
Kwa sasa familia hiyo ambayo imelaani kitendo hicho inataka serikali kuingilia kati kujua kilichsabibisha kifo hicho na kunusuru watoto wanaougua hospitalini ili kuzuia maafa zaidi.
By James Shitemi