by Musa Brian
Mwanaume mwenye umri wa miaka 30 , kutoka eneo la shikuhula , kaunti ya kakamega , ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kuiba ng’ombe , majira ya usiku.
mwathiriwa Wilson Kethi ambaye ni mwenye ngombe huyo alipiga ripoti kwa kituo cha polisi cha lubao , ambapo naibu chifu wa kata ndogo ya lubao suluvei shihafu ashiono alichukua hatua .Mwathiriwa wilson keth aeleza ni kipi kilichotukia wakati alipogundua kuwa ameibiwa .
Akithibitisha kisa hicho baada ya kumtia mbaroni mshukiwa huyo katika kituo cha polisi cha lubao , Bi Suluvei Shihafu Ashiono alisema kuwa mshukiwa ametiwa mbaroni na maafisa wake, kwa ushirikiano na nyumba kumi wa eneo hilo.
Hata hivyo Bi. Suluvei ameomba wenyeji kutochukua hatua za kisheria mikononi mwao kwani kunavyo vitengo vilivyo pewa wajibu wa kutekeleza sheria .