Maafisa wa polisi mjini Kakamega wanachunguza kisa ambacho mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha masinde muliro anadaiwa kuavya mimba kabla yakutupa kijusi kwenye kichaka katika Mtaa wa kefinco wadi ya shieywe viungani mwa mji wa Kakamega.
Kulingana na walioshuhudia kisa hicho wanadai kuwa msichana huyo aliavya mimba hiyo ya miezi Saba kabla yakutupa kijusi huyo kwenye kichaka kilicho karibu ambapo alipatikana na wenyeji baada ya wazazi wake kuripoti kitendo hicho.
Hata hivyo wenyeji wa Mtaa huo wamelaani kitendo hicho huku wakisema kuwa visa vya wanafunzi kuavya mimba zimeenea sehemu hiyo na kuwataka watoto wa kike kuwacha kufanya mapenzi kiholela holela pasipo kujitayarisha
Ripoti ya Richard Milimu