15/8/20 JUMAMOSI
Mhudumu mmoja wa pikipiki na abiria wawili akiwemo mwanamke wamefariki papo hapo baada ya kuangukiwa na lori Aina ya Trela iliyokuwa imebeba miwa kuelekea kiwanda cha kusaga miwa cha west kenya eneo la Kisumu ndogo eneo bunge la malava kaunti ya Kakamega.
Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo wanasema kuwa dereva wa Lori Hilo alikuwa akiliendesha Kwa mwendo wa Kasi kabla ya kukosa mwelekeo na kuangukia watu hao watatu.Hata hivyo wananchi wenye ghadhabu waliteketeza trela Hilo pamoja na gari la kuzima Moto la kampuni hiyo.
Miili ya watatu hao imepelekwa kwenye hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya Kakamega.