Mabingwa watetezi katika msururu wa raga nchini KCB RFC wanawania kuibuka mababe katika awamu ya raga ya wachezaji saba kila upande ya CHRISTIES. KCB wako katika kundi A pamoja na wenyeji Kenya Harlequins, Top Fry Nakuru na Jumia Pay Pirates ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano haya. Chuo kikuu cha Strathmore ambao walitinga fainali ya awamu iliyopita ya Kabeberi kwa upande wao watakuwa makini kuendeleza matokeo yao bora. Strathmore itajipima nguvu dhidi ya Impala Seracenes, Black Blad na chuo kikuu cha Daystar katika kundi B.

Mabingwa wa ligi kuu ya raga Kabras Sugar wako katika kundi C pamoja na chuo kikuu cha Masinde Muliro, Menengai Oilers na Nondescript. Kundi D limewabeba Homeboyz, Catholic Monks, Mwamba RFC na Western Bulls. Wapenzi wa raga wanatarajia kuwa na shindano la kukata na shoka katika awamu hii ya msururu wa raga.

Related Post

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE