Mbiu la manjonzi limetanda katika shule ya upili ya Arnesense baada ya mwanafunzi wa kidato Cha kwanza kufariki katika mazingira tata.

Wakaazi kutoka eneo la Burnt Forest wamesema kuwa mwanafunzi huyo anadaiwa kufariki na homa ya korona.

Maisha ya wakazi hao yamo hatarini baada ya shule hiyo kufungwa kabla ya kupima dhidi ya Ugonjwa huo na kuwapa chanjo kwa wanafunzi hao.

Juhudi za kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule ya Arnesense hazijafua dafu.

Kaunti kamishina wa kaunti ya Uasin Gishu alithibitisha kisa hicho kwa njia ya simu na kusihi kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kubaini chanzo cha mwanafunzi kufariki.

By Sharon Lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE