Polisi jijini Nairobi wanamzuilia mwanamke mmoja anayedaiwa kumuua mumewe kwa kumdunga kisu kufuatia mzozo wa kinyumbani .
Peninah Wanjiru wa miaka 33, anadaiwa kutoa kisu na kumdunga mumewe George Ogamo wa miaka 27, kisha kujaribu kutoroka walipokuwa wanazozana nyumbani kwao katika kijiji cha Mukarara eneo la Dagoretti, Nairobi.
Polisi waliweza kumkamata mshukiwa kutoka mafichoni maeneo hayo ya Dagoretti na kumzuilia
Bado haijabainika wazi kiini cha mzozo uliosababisha maafa hayo huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika ili kupata majibu.
By Imelda Lihavi