Maafisa wa polisi mjini Cheptais eneobunge la Mlima Elgon wanamzuilia mwanamume mmoja mwenye umri wa makamo baada yake kupatikana akiwa amejifungia na mtoto wa kike mwenye umri wa miaka kumi na tano kwenye chumba kimoja eneo la Bukonoi kwenye kata ya Sasur.

Kulingana na naibu chifu wa kata ndogo ya Toroso eneobunge la Mlima Elgon Titus Cheshari alifahamishwa na mzee wa kijiji cha Bukonoi kuhusu tukio hilo ambapo alimfumania mshukiwa huyo Wilson Barasa mwenye umri wa miaka ishirini na tano akiwa amejifungia ndani ya chumba na mtoto huyo.

Aidha Cheshari anasema  aliwafahamisha maafisa wa polisi  ambao walimkamata mshukiwa huyo na kuwapeleka wawili hao kwenye hospitali ya kaunti ndogo ya Cheptais, kufanyiwa vipimo vya matibabu kabla ya kumzuilia Barasa kwenye kituo cha polisi cha Cheptais.

Cheshari amewataka wazazi kuwapa wanao malezi bora huku maafisa wa polisi wakiendeleza uchunguzi  kufwatia tukio hilo.

Yanajiri haya siku chache baada ya naibu chifu wa kata ndogo ya Sasur kufikishwa mahakamani kwa kudaiwa kumnajisi mtoto wa miaka kumi na saba kwenye chumba kimoja kwenye soko la Cheptais huku mwanamume mwingine   kukamatwa kwa kudaiwa kumnajisi kisha kumuuwa mwanafunzi wa shule ya msingi ya Kapsoromet miezi mitatu iliyopita.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE