mwanamme mmoja mwenye  umri wa makamo mkaazi wa kijiji cha  Kamagambo  kaunti ya Kirinyaga ameharibu mali iliyokuwa na dhamana  ya shilingi takribani milioni mia mbili baada ya mkewe kusistiza kwenda sokoni siku ya Jumapili.

 Kulingana na walioshuhudia,mwanaume Yule alitumia panga kukatakata ndizi na pia Avocado zilizokuwa kwenye magunia kadhaa na kusema kuwa mkewe alistahili kukaa nyumbani kwani ilikuwa siku yakina baba ulimwenguni.

Kulingana na majirani waliozungumza na vyombo vya habari ,mwanamke huyo huishi kwa kutegemea mapato kutoka kwa kuuza mazao ya shamba katika soko la Kitui siku za Jumapili

Hellen Kaari Muriithi,mmoja wa wale mali yao iliharibiwa, alisema kuwa wanabodaboda walimweleza kuwa walimuona mtu akiharibu mali yake.na walipofanya uchunguzi walipata kuwa Yule aliyehusika  ni mume wa mmoja wa wale ndizi yao Ilikuwa Imeharibiwa.

Mary Owano

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE