Polisi wa Khwsero wanamzuilia mwanamume wa miaka 32 kwa kudaiwa kumnajisi msichana wake wa miaka kumi na miwili mwanafunzi wa darasa la sita katika kijiji cha Emung’weso kata ndogo ya Shirali

 Chifu wa kata ya Mulwanda Paul Ochango amesema walipata ripoti kutoka kwa walimu na baada ya msichana huyo kupokea matibabu, waliweza kumkamata babake ambaye wamekuwa wakiishi naye baada ya kutengana na mkewe

Chifu Ochango anawataka akina mama kuwajibikia watoto wao wanapotengana na waume wao badala ya kuwaacha na waume wao

Naibu Chifu alielezea kua “Nilipata habari kwamba alikua amenajisi mtoto wake wa miaka 12. Antony Were ambaye ni babake huyu mtoto ana miaka 32. tulichukua mtoto na tukampeleka hospitali na tukapata amenajisiwa. Mtoto ameeleza kuwa alikua akinajisiwa kila wakati na kulingani na majirani pia walisema walimuogopa mwanaume huyo na hawakuweza kumuokoa mtoto huyo na pia hawangeweza kuripoti” Story by Boaz Shitemi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE