Hali ya uzini ingali imetanda katika kijiji cha Mang’ang’a wadi ya Isukha Kaskazini eneobunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega baada ya mwili wa mwanaume mmoja Peter Mbalilwa aliyetoweka siku ya jumapili katika njia ya kutatanisha kupatiikana kupatikana ndani ya miwa akiwa amefariki.
kwa mjibu wa Adanasi Mwisai na Judithi Musanga wazazi wa mwendazake ni kwamba mwendazake aliondoka nyumbani siku ya jumapili baada ya kutoka kanisani huku juhudi za kumpata alikokwenda zikigonga mwamba na baadaye mwili wake kupatikani ndani ya miwa ya jirani
kisa hicho kimedhibitishwa na mwenyekiti wa nyumba kumi Charlse Shihoya huku mwili wa mwendazake ukihifadhiwa katika hifadhi ya wavu ya hospitali ya rufaa ya Kakamega ukisubiria kufanyiwa upasuaji hili kubaini chanzo cha mauti hayo.