Coronavirus COVID-19 single dose small vials and multi dose in scientist hands concept. Research for new novel corona virus immunization drug.

Huku zoezi la chanjo dhidi ya virusi vya korona ikiendelea, wito unazidi kutolewa na viongozi mbalimbali kuwahimiza wanainchi kujitokeza ili kupokea chanjo hiyo.

Wa hivi punde kuzungumzia swala hilo ni askofu wa kanisa la Holy Gate of Heven mjini Bungoma Alex Lwamba, katika kikao na wanahabari ofisini mwake askofu Lwamba amesema kuwa ni vyema watu kuondoa uoga na dhana potovu dhidi ya chanjo hiyo, kwani hii ni kwa manufa ya afya yao wenyewe.

Alex pia amesema kuwa ni vyema wazazi kuwalea wanao kwa misingi ya kikirsto, jambao ambalo litawezesha wanao kuwa na madili mema katika jamii.

Aidha amekashifu wasani chipukizi wanao imba nyimbo za injili, kuwa baadhi ya nyimbo hizo hazina ujumbe mwafaka na unaodhihirisha wakovu.

Vilevile askofu huyo ametoa wito Kwa wale wanaotumia mitandao za kijami, kuzitumia vizuri hata kusikia mahubiri Kwa minajili ya manufa yao bali si kutazama video ambao itaweza kuwapotosha.

By  Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE