Kuna takribani miaka minne hadi uchaguzi mkuu wa Tanzania wa 2025. Ni muda mrefu kwa hakika. Wakati vyama vya upinzani havijawaza hata kuwasaka wagombea wao wa urais, chama cha mapinduzi (CCM) kinaonekana tayari kimekwishakumfahamu nani ataipeperusha bendera yao katika mwaka huo.

Hali hii inakuja baada ya kile kinachoweza kuitwa taarifa ya uzushi iliyoandikwa na gazeti kongwe la uhuru, linalomilikiwa na CCM, likieleza rais Samia hana nia ya kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao. Sasa rais mwenyewe ameibuka na kuweka bayana nia ya kutaka muhula wa pili.

Kauli yake ni ya kisiasa zaidi, imebeba maneno yenye kuashiria kana kwamba ana uhakika na ushindi. Ingawa hilo ni kawaida panapohusika tambo za kisiasa. Hatima ya tambo hizo huwa ni kura kisandukuni

By Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE