Muungano wa kiuchumi Kaskazini mwa Bonde la Ufa ikishirikiana na kiwanda cha ( Fresh Produce Consortium of Kenya) itaanza rasmi kilimo cha maua kwa kuuza bidha zao nchi za nje kuanzia wiki ya kwanza ya machi mwaka huu. Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha (Fresh Produce Consortium) Okisegere Ojepat amesema kuwa kwa kutumia kiwanja cha ndege mjini Eldoret itawasaidia kwa kusafirisha bidhaa hizo kwa nchi za nje na italeta manufaa hasa kwa wakulima. Hata hivyo amewashauri wakulima kutoka kaunti za Noreb na hata pia kaunti ya Turkana kuendelea kujihusisha kwa kilimo. Wakati huo huo naibu gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Daniel Chemno amesihi kuwa bali na janga la korona kuibuka .mwaka wa 2020 waliweza kuuza bidhaa zao kwa nchi za nje kwa wingi hasa wakilinganisha na mwaka wa 2019 aidha,  amewashauri wakulima kuendeleza kilimo kwani watafaidika kifedha na kujikimu kimaisha. Hata hivyo mkurugenzi mtendaji wa muungano wa kaskazi mwa bonde la ufa Noreb Dominic Biwott ametoa wito kwa serikali kuweza kuboresha miundo mbinu ya Kenya Port Authority mjini Eldoret. Story By Sharon Lukorito  ReplyForward

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE