Ugavi wa nyadhifa za uongozi katika chama cha ODM kwenye kaunti ya Kakamega sasa unatishia uthabiti wa chama hicho baada ya baadhi ya viongozi kulalama maeneo yao kutengwa kwenye ugavi wa nyadhifa hizo.

Viongozi wa chama hicho kutoka maeneo bunge ya Mumias Magharibi na Matungu wameelezea kutohusishwa na jinsi zoezi la ugavi wa  nyadhifa hizo lilivyoendeshwa na nafasi walizopewa.

Wakiongozwa na aliyekua mwakilishi wa wadi ya Mumias ya kati Suleiman Odanga na katibu Razia Makokha, wamewasuta baadhi ya maafisa katika afisi ya gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya kwa kuitilafiana na zoezi hilo

Wakiwahutubia wanahabari mjini Mumias, viongozi hao wamemtaka gavana Oparanya kutofumbia macho swala hilo wakidai chama chao kimetekwa nyara na baadhi ya watu ambao lengo lao ni kuona chama cha hicho kinapoteza umaarufu mbele ya uchaguzi mkuu ujao.

Kwenye orodha ya uongozi mpya wa chama hicho, mbunge wa Shinyalu Justus Kizito atakua mwenyekiti wa chama, mwakilishi wa wadi ya Malaha Isongo Makunga Lucas Radoli Ochami akiwa naibu wake, nabii Nabwera akichukua wadhifa wa katibu huku Mophat Mandela akiridhika na wadhifa wa kiongozi wa vijana miongoni mwa nyadhifa zingine.

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE