Kasisi mkuu kanisa la Baptist mjini Bungoma Clapperton Mchanga amewarai viongozi nchini kuwa na mshikamano tunapoelekea uchaguzi mkuu mwakani.
Akizungumza kwenye hafla ya maombi kanisani mwake mjini Bungoma kasisi huyo amesikitikia vuta ni kuvute za kisiasa za viongozi wa haiba ya juu nchini zinazoendelea kushuhudiwa huku akitilia hofu kuwa huenda zikaleta migogoro ya kisiasa nchini.
Kasisi Clapperton amehoji kuwa ni wajibu wa kila kiongozi kuheshimu ajenda za mwenzake huku akisema kuwa siasa za viama zilibuniwa kuleta uiyano na demokrasia wala sio kugawanya wana nchi kama inavyoshuhudiwa kwa sasa.
Mtumishi huyo wa Mungu aidha ameitumia fursa hiyo kuwatahadharisha viongozi wenzake wa kidini na vijana dhidi ya kujihusisha na siasa za kimirengo na matusi kama mojawapo wa njia za kupunguza joto la kisiasa nchini.
Ikumbukwe kuwa siku za hivi karibuni viongozi wakuu serikalini akiwemo naibu wa rais DKT William Samoei Ruto na waziri wa usalama wa ndani daktari Fred Matiangi wameonekana kutofautiana hadharani kutokana na swala la haswaa ni nani anafaa kuwekea ulinzi naibu wa rais William Ruto swala ambalo limeonekana kuuzambaratisha hata zaidi uhusiano kati ya rais Kenyatta na naibu wake.
By Hilary Karungani