Huku serikali na mashirika ya kijamii yakiendeleza vita dhidi ya mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi wa kike, imebainika kuwa wahusika wa kiume wa mimba hizo ndio huathirika zaidi kuliko wenzao wa kike, baadhi yao wakijipata na magonjwa ya kiakili na hata kupoteza maisha.

Shirika la vijana la Siki Youth Association limefichua kuwa, mvulana anapompachika msichana mimba husongwa na mawazo zaidi ya msichana mja mzito na hivyo kuathirika na maradhi ya kiakili ambayo inaweza kumweka hatarini iwapo hatapata ushauri nasaha.

Emmah karanja ni mwazilishi wa shirika la  siki shirika linaloshugulia maswala ya vijana katika jamii.

Karanja aidha anasema swala hili litapata suluhu iwapo tu jamii itashirikiana kuondoa unyanyapaa na msongo wa mawazo miongoni mwa vijana, ili kuwaepusha kwenye hatari ya kupata marathi ya kiakili ambayo inaweza kusambaratisha maisha yao.

Ni kauli iliyosisitizwa na afisa katika shirika hilo Aisha Ahmmed  

wameyasema haya katika shule ya msingi ya Esirisia eneo bunge la Matayos kaunti ya Busia kwenye hafla ya kuhamasisha jamii kwa lengo la kuwashauri vijana kuhusiana na changamoto kadha za kimaisha.

By Hilary karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE