Mwanaharakati wa maendeleo eneobunge la Bumula kaunti ya Bungoma Jack Wanami ametoa wito kwa walio na uwezo katika jamii kuwafaa wasiojiweza na kuwainua kimaisha
Akizungumza katika eneobunge lake Wanami amesema kuwa akishirikiana na washikadahu mbalimbali watahakikisha kuwa wakaazi wote wasiojiweza wanapokea huduma za afya kupitia hazina ya matibabu nchini NHIF
Amehoji kuwa wanao mpango vilevile wa kuwapa elimu watoto kutoka familia zisizo jiweza akiwashukuru washirika wakiwemo vyongozi wa kisiasa wanaokumbatia mpango huo
Mwanaharakati huyo anayekimezea kiti cha eneobunge la Bumula amepuuzilia mbali madai kuwa polisi wanatekeleza majukumu yao kimapendeleo haswa kwenye vita dhidi ya ugonjwa wa covid 19 akiwataka wapinzani wake kuzingatia ajenda kwa wakaazi wala sio uvumi
By Imelda Lihavi