Vituo vitano vya kuwashughulikia wahasiriwa wa dhuluma za kijinsia vimezinduliwa rasmi kaunti ya Kakamega  na nia ya kukabili visa hivyo vilivyoenea kaunti hiyo huku serikali ya kaunti ikiendeleza juhudi za kukamilisha mswada utakaohakikisha kuwa wote wanaowadhulumu wenzao kijinsia kaunti hiyo wanakabiliwa na mkono wa sheria.

Daktari msimamizi katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kakamega Victor Dzimbulu amekiri kuwapokea wagonjwa wengi kutokana na visa vya  dhulum za kijinsia  na kueleza kuwa  asilimia 70 ya wahasiriwa huwa haijitokezi kuripoti visa hivi  wala kutafuta matibabu, akiitaka jamii kuhakikisha kuwa visa hivi vinaripotiwa ili wahasiriwa wapate usaidizi.

  Vituo hivi vimo katika maeneo bunge tofauti ya kaunti ya Kakamega  na vinalenga kuwasaidia wote walioathirika huku serikali ya kaunti yua Kakamega ikiwa mbioni kuhakikisha kuwa kuna sheria itakayokabiliana na wahusika.

Hapo awali wahasiriwa walilazimika kurejea katika jamii mara tu baada ya kupokea matibabu kabla ya kupewa mawaidha ya kutosha kukabiliana na yaliyojiri pamoja na unyanyapaa kwa kukosekana kwa vituo vya kuwasidia.

Ni ufadhili kutoka kwa shirika la usaid kwa serikali ya kaunti ya kakamega, na hapo awali shirika hili lilitoa magari matatu kwa ajili ya kuimarisha afya ya uzazi kaunti hii ya Kakamega.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE