Serikali ya kaunti ya Kakamega imeanzisha mchakato wa kuwahamasisha wakulima wa kaunti hiyo kuhusu kilimo cha samaki na nia ya kukiimarisha kilimo hicho ili kuinua kiwango cha uchumi miongoni mwao.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo katika boma la mkulima mmoja maeneo ya Shisiru wadi ya Butsotso ya kati eneo bunge la Lurambi, afisa inayesinamia idara ya ufukaji wa Samaki kaunti ndogo ya Lurambi Japheth Juma amesema kuwa serikali ya kaunti hiyo imejitolea kuwawezesha wakulima hao kwa kuwapa mahitaji yanayofaa kilimo hicho.
Wakati huo uo afisa huyo amedokeza kuwa eneo hilo liko na uwezo wa kukuza Samaki kwa wingi huku akiwataka wakulima kukumbatia mradi huo ambao serikali inapeana ufadhili wa asilimia 50 kupiga jeki kilimo hicho .
Kwa upande mwingine wakulima waliohudhuria mafunzo hayo walipongeza serikali kwa kuanzisha mradi huo wa samaki na kutaka wengine ambao bado hawajajiunga kufanya hivyo ili waweze kung’atuka katika lindi la ufukara .
By Imelda Lihavi