Watu watano wakiwemo baba, mama na wanao wawili wamelazwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya waliyoyapata baada ya trela moja lililokuwa likisafiri kwenye barabara kuu ya Eldoret – Webuye kupoteza mwelekeo na kuingia kwenye jengo moja katika eneo la Mwamba eneo bunge la Lugari kaunti ya Kakamega. 

Kulingana na majirani,  waliusikia mshindo mkuu walipoenda kutazama walilipata trela hilo likiwa limeingia na kuanguka ndani ya nyumba anamoishi ya bw. John Kisiangani Muyaka na jamii yake. 

Juhudi za pamoja za majirani zilifanikiwa kuwaokoa kisiangani,  mkewe diana naswa ambaye ni mja mzito, wanao wawili pamoja na dereva wa trela hilo na kuwakimbiza katika hospitali ya kaunti ndogo ya Turbo kabla ya kusafirishwa hadi hospitali ya rufaa ya Moi mjini Eldoret ambako wamelazwa.

Jamii  ya wahasiriwa ikiongozwa na David Wamalwa imeelezea kusikitishwa kwake na kisa hiki  na kuomba msaada.

Inadaiwa trela hilo lilikuwa likisafirisha cha kula cha msaada kutoka shirika la Umoja wa Kimataifa kabla ya kutokea kwa ajali hiyo.

Kisa hiki kimethibitishwa na kinara wa polisi katika kaunti ndogo ya Lugari Bernard Ngungu.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE