Kumeshuhudiwa mvutano baina ya baadhi ya wakilishi wadi na polisi nje ya majengo ya bunge la Kaunti ya Bungoma, baada ya wakilishi wadi hao kufika katika bunge hilo na kupata limefungwa wakizuiwa kuingia ndani ili kujadili mswada wa bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2021/22.

Wakilishi wadi hao zaidi ya Ishirini wanamtaka Spika was bunge hilo Emmanuel Situma na karani wa bunge hilo John Mosongo kutimuliwa mamlakani.

Aliyekuwa Naibu Spika wa bunge hilo ambaye pia ni Mwakilishi wadi ya Siboti Wamusai Simiyu akisema bunge hilo limefungwa kwa zaidi ya wiki mbili sasa bila sababu muhimu.

Hata hivyo wamewakosoa polisi kwa kuingilia shughuli za bunge hilo wakiwataka badala yake kumtafuta alipo spika Emmanuel Situma na kumwasilisha bungeni ili afungue bunge hilo kuruhusu kurejelewa shughuli zake jinsi anavyoeleza Paul Wanyoike ambaye ni mwakilishi wadi ya Matulo katika eneo bunge la Webuye Magharibi.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE