Wazazi kutoka kaunti ya kakamega na maeneo mengine nchini walio na watoto wanaosikia na kuona ,japo wanamatatizo ya kiakili wametakiwa kuwapeleka wanao katika shule ya shavihiga special school iliyo wadi ya Idakho Mashariki eneo bunge la Ikolomani kaunti ya Kakamega,bali na kukaa nao nyumbani bila kuwashugulikia.
Mwalimu mkuu wa shavihiga special school, Damary Otieno anasema kufikia sasa watoto ambao wamejiunga na shule hiyo wamesaidika kwa kupata ujuzi mbali mbali.
Damary otieno amewataka wahisani kuzidi kujitokeza kusaidia watoto wa shavihiga special School ili wapate vifaa vya kusomea chakula na vifaa vya kujifunza mambo ya ushonaji ,kunyoa na ususi.
Shule ya Shavihiga Special School ina wanafunzi 130, kufikia sasa ,huku ikiwa na nafasi kwa wale wakuishi shuleni na kwenda nyumbani.
Na Kennedy Babangida