Wakaazi wa mlima elgon wametoa makataa ya siku saba kwa gavana wa kaunti ya Trans Nzoia George Natembeya kuwaomba msamaha kwa matamshi yake kuwa hawawezi pata kaunti yao kutokana na uchache wao. Kulingana nao, siku saba zikitamatika kabla ya kupokea ridhaa kutoka kwa Gavana Natembeya wataandamana hadi makao makuu ya gavana huyo mjini kitale
Wakaazi hao wakiongozwa naye Michael Maruti wakizungumza mjini kapsokwony wametoa ilani kwa Gavana Natembeya kwa kile wanachodai ni kudhalilishwa nakukosewa heshima huku wakimtaka kuwaongoza wananchi kwa njia iliyo bora.
Ni usemi ulioungwa mkono naye aliyekuwa diwani Joseph Ngomat anayesema kuwa huwenda matamshi hayo yakachochea ukosefu wa usalama au vurugu
Kwa upande wao vijana wameelezea manufaa ambayo watapata iwapo eneo bunge la mlima Elgon litapewa kaunti baada ya mswada huo kupitishwa bungeni huku akina mama wakitishia kumulaani gavana huyo
Na Everlyne Wanjala