Gavana wa kaunti ya Kakamega Fernandes Barasa ameshikilia msimamo wake wa kushirikiana na serikali kuu ya Rais William Ruto licha ya kuwa katika mrengo wa upinzani azimio
Ameyasema hayo baada ya kuhudhuria ibaada ya jumapili katika kanisa la Church Of God Mwihila wadi ya Kisa Kaskazini eneo Bunge la Khwisero
Barasa amesema kuwa Rais William Ruto atazuru kaunti ya Kakamega kwanzia alhamisi tarehe 8 huku akiahidi kushirikiana naye kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo hospitali ya level 6 iliyoanzishwa na mtangulizi wake Wycliffe Oparanya
Wakati uo huo Barasa akipongeza uamuzi wa chopokazi la kupiga msasa mtaala mpya wa elimu nchini CBC kwa kuamua wanafunzi wa gredi ya sita kusalia katika shule za msingi
Akipongezea hatua pia ya katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi nchini Francis Atwoli kuridhiana na Rais William Ruto kwa faida ya wafanyakazi anaosimamia
Barasa ameitaka hazina kuu ya serikali kuachilia mgao kwa serikali za ugatuzi kwani kufikia sasa mgao huo haujafikia kaunti huku wanainchi wakitarajia miradi ya maendeleo kutoka kwa magavana
Ameahidi pia kuboresha sekta ya afya kwa maeneo bunge yote 12 ya kaunti ya Kakamega akitaka ushirikiano uwepo baina ya serikali ya kaunti na wasimamizi wa hospitali mbalimbali ili kumaliza kero haswa la kukosekana kwa dawa katika vituo vya afya
Sajida Javan