Viongozi mbalimbali kutoka eneobunge la Mumias Mashariki wanazidi kulalamikia utovu wa usalama ambao umekithiri eneo hilo
Mwanasiasa Paul Makokha amekuwa wa hivi punde kushtumu hali hii akilaumu idara ya usalama eneo hilo kwa utepetevu
Makokha amesema kuwa huwenda polisi wanashirikiana na wahalifu kuwahangaisha raia akishangaa mbona wezi hao hawakabiliwi kisheria
Kiongozi huyo amesikitikia kiwango cha juu cha fedha zinazotengewa idara hiyo ilihali wakaazi wanazidi kuishi kwa hofu akiongeza kuwa hili pia ni tishio kwa wawekezaji
By James Nadwa