Mwakilishi maalum katika bunge la kaunti ya Kakamega Lucy Chogo amewahimiza wakazi kushirikiana na mashirika yanayolenga kuboresha hali ya maisha kweza kujiendeleza
Akiongea eneo la Makhokho Idakho Mashariki eneo bunge la Ikolomani wakati wa kukabidhi shilingi milioni moja na laki nane za kusaidia elimu ya wanafunzi kutoka shirika la Shining Hope For Communities, bi Chogo amesema kuna mengi ambayo yataafikiwa ikiwa vikundi zaidi vitajiunga na mashirika kama haya
Aidha bi chogo amewahimiza wazazi hasa akina mama kukumbatia miradi ya kuboresha mapato ili kurahisisha usaidizi kutoka kwa viongozi
By Lindah Adhiambo