Serikali ya kaunti ya Kakamega inafanya kila iwezalo kuzisaidia kamati simamizi za masoko sehemu mbalimbali katika kaunti hiyo kama njia mojawapo ya kuimarisha masoko hayo
Kwenye mahojiano ya kipekee na idhaa hii mshauri serikali ya kaunti ya Kakamega kuhusu uongozi Ali Musa Chibole hata hivyo ametaja kucheleweshwa kwa pesa kutoka serikali kuu kumeathiri usimamizi huo
Chibole amesema kuwa kama serikali wanajaribu kutatua tatizo hilo
Chibole aidha amekiri kuwepo kwa changamoto katika kurekebisha miundomsingi haswa daraja zinazosombwa na maji ila ameahidi swala hilo kuangaziwa hivi punde.
Haya yanajiri huku daraja kadhaa eneobunge la Mumias Mashariki zinazounganisha kaunti hiyo ndogo na Ile ya Lurambi pamoja na ya Butere kwenye mitaa ya Maraba-Matende na Isango -Esokone zikisalia kusombwa na maji
Mshauri huyo wa Gavana aliwataka wakaazi kumchagua kiongozi atakaueendeleza maono ya Gavana Oparanya baada ya kipindi chake kutamatika
By James Nadwa