Vijana katika eneo la Marama Kaskazini eneo Bunge la Butere kaunti ya Kakamega wamewataka viongozi waliochaguliwa kushirikiana na idara ya usalama kukabili
ongezeko la visa vya wizi wa mifugo
Wakiongozwa na Edwin Anyanga baada ya kuhudhuria mazishi eneo la Bumamu wamesema wizi wa mifugo umechangia hali ya ufukara huku viongozi waliochaguliwa wakikosa Kuwajibikia hali hiyo.
Wizi wa mifugo umezidi katika eneo hili. Na hii wizi imechangia umaskini Kwa sababu mtu akishaa kuibia ng’ombe mbuzi kondoo kuku anaacha mwenye mifugo bila kitu na tunaomba serikali kuingilia kati na kudumisha usalama eneo hilo na hata viongozi wetu kama MCA pia mueze kuingilia kati.
By Lindah Adhiambo