Zaidi ya wanafunzi hamsini kutoka kijiji cha Kototoi kule Ang’urai kaunti ndogo ya Teso Kaskazini kaunti ya Busia, wamepokea ufadhili wa masomo kuwawezesha kujiunga na shule za upili na vyuo vikuu, kutoka kwa shirika moja la kijamii linalojishugulisha na utunzi wa mazingira kwa jina [Lakajokan- C.B.O], shirika hilo pia likiwajengea wazazi wao nyumba ya mabati.

Mkurugenzi wa shirika hilo Daniel Okapes, mshirikishi Pamela Oduya na naibu mwenyekiti Moses Omunyin, wanasema waliafikia hatua ya kuelimesha vikundi vya akina mama namna ya kulinda mazingira hatua hiyo ikilenga kupunguza hali ya umaskini kwa jamii.

Benina Nekesa, Ann Onyapidi na Mukanda Saum ni miongoni mwa wanachama wa Lakajokan C.B.O kutoka Katotoi, wanasema mbali na msaada wa nyumba na ufadhili wa masomo kwa wanao pia wamenufaika na mahitaji mengine ya kimsingi.


Mradi huo vilevile ukipunguza visa vya utovu wa nidhamu miongoni mwa vijana kwani vijana wengi wamepata ajira huku wakiepukana na utumizi wa mihadarati.

Wasimamizi wa mradi huo wamempongeza mbunge mwakilishi wa akina mama kaunti ya Busia Bi Florence Mutua kutokana na juhudi zake za kupiga jeki mradi huo huku wakitoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano wake.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na mkurugenzi mkuu wa kikundi cha kutunza mazingira cha Linda Mazingira Patrick Ikwara ambaye amesema serikali inalenga kupanda miche milioni 43 kwenye bajeti ya mwaka wa kifedha 2021-22.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE