Kaunti ndogo ya Kirima katika kaunti ya Laikipia imebuniwa na waziri wa usalama wa taifa Dkt Fred Matiang’i. Kaunti hiyo ndogo imebuniwa ili kusaidia kukabiliana na utovu wa usalama katika eneo hilo. Tangazo hilo liliwekwa kwenye gazeti la rasmi la serekali toleo la tarehe tisa mwezi Septemba mwaka wa 2021

Wazili wa usalama pamoja na maafisa wengine kutoka vitengo mbalimbali vya usalama wamekua kaunti ya Laikipia kukagua usalama na kuwasaka majambazi wanao wahangaisha majambazi

Waziri Matiang’i anatarajiwa kutangaza mabadiliko akiwa katika eneo hilo katika harakati za kukabiliana na zimwi hilo la ukosefu wa usalama linaloghubika Laikipia.

Familia zaidi zinaendelea kutoroka eneo hilo kutokana na hofu ya kushambuliwa huku serikali ikiahidi kusaidia familia hizo kuanza upya maisha yao.

Inspekta Jenerali wa polisi Hillary Mutyambai amewahakikishia wakenya kwamba hali ya utulivu itarejeshwa katika eneo hilo katika muda wa Juma moja.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE