Makadirio ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2021/2022 yanayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hapo kesho na waziri wa fedha Ukur Yatani yanasemekana huenda hayatakuwa ya afueni kwa wakenya, hasa mkenya wa kawaida.

Aliyekuwa wakati mmoja waziri wa fedha, kiongozi wa chama cha ANC, Musalia Mudavadi amesema kuwa madeni ambayo kenya kama taifa imekopa hadi kufikia sasa ni mojawepo ya sababu kuu ambazo zitachangia kuwepo kwa wakati mgumu kuafikia utekelezaji wa bajeti hii ambayo inakisiwa itagharimu hadi kiasi cha shilingi trilioni 3.6 pesa za kenya.

Akizungumza hii leo, siku moja kabla ya kusomwa kwa makadirio hayo ya bajeti, mudavadi amesema kuwa changamoto zilizoibuka kutokana na athari za janga la covid, zimetonesha kidonda zaidi kwani tayari hali ya kiuchumi nchini ilikuwa inayumba yumba suala ambalo pia limeathiri pakubwa uekezaji humu nchini pasi na biashara kuathirika pakubwa na hata zingine kfungwa kwani mataifa ya nje vile vile yana changamoto zake kutokana na janga hili la covid na kwa sasa hamna msamaria mwema ambaye kenya yaweza kimbilia ili kuapata afueni.

Ikisubiriwa kuona ni vipi bei ya bidhaa za kawaida za matumizi ya nyumbani kila siku na hasa vyakula itakavyokuwa kutokana na makadirio ya bajeti hii, huenda hali ikazidi kuwa ngumu zaidi anavyoelezea mudavadi.

Macho yote hapo kesho yakiwa kwa waziri wa fedha Ukur Yaatani, huku serikali ya rais uhuru kenyatta pia ikimulikwa kwa karibu na wananchi kuona mabadiliko baada ya kupasishwa kwa bajeti hii yatakuwa ya manufaa kwa mwananchi wa kawaida au iwapo utakuwa basi tena msumari moto kwenye kidonda.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE