Hali ya hofu imetanda eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega baada ya afisa mmoja wa Msitu wa Kakamega kuuwawa kwa kukatwakatwa kinyama na wenyeji ndani ya msitu maeneo ya Iloro huku wenzake wawili wakinusurika kifo.

Wenyeji waliofika eneo la mkasa  wanasema  kuwa mwendazake akiwa na wenzake walipata wenyeji wakichunga mifugo na kuokota kuni  kwenye msitu huo na kuanza kuwakimbiza wenyeji hao hadi kwenye maboma zao zilizokaribu na msitu huo kabla ya wakazi hao kuwageuka  kwa kuwashambulia kwa panga na kumuua mmoja wao.

Hata hivyo wenyeji hao wakiongozwa na Edwin Musungu wanadai kuwa maafisa hao wamekuwa na tabia ya kuhangaisha wakazi wanapotafuta kuni kwenye msitu huo wakiwemo akina mama.

Kwa upande wake mbunge wa Shinyalu Kizito Mugali akikashfu visa vya wakazi kuwangaishwa na maafisa hao kila kukucha.

Kamanda wa polisi wa Shinyalu Robert Makau amethibitisha kisa hicho akihoji kuwa mwendazake pamoja na wenzake walikuwa kwenye patroli kabla ya kukumbana na mauti ya mmoja wao huku akisema kuwa marehemu alifariki kwa kutokwa na damu nyingi iliyotokana na majeraha ya kukatwa.

By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE