Baadhi ya wawakilishi wadi katika kaunti ya Kakamega  wameunga mkono masharti ya rais Uhuru Kenyatta ya kudhibiti corona na kuendeleza kampein za kuwahamasisha wananchi kuelewa na kuunga mkono maelekezo ya rais kuona kwamba corona inazuiwa

 Mwakilishi wadi ya Mumias Mashariki Shabaan Otengo ambaye alihudhuria mazishi eneo la Emahola katika wadi yake amewataka wananchi na viongozi kuzingatia masharti yaliyotolewa na rais na wawache kuhatarisha maisha yao na ya wengine

Otengo vile vile ameitaka serikali kusambaza chanjo ya kutosha mashinani huku akiwarai wananchi kutopotoshwa na wanasiasa na kupuuza maagizo ya afya

Otengo ametumia fursa hiyo kuwataka wakuu wa shule kutowatuma nyumbani wanafunzi hasa baada ya kutoa fedha za kuwasaidia wanafunzi wenye changamto za kifedha kutoka kwa serikali ya kaunti

BY James Shitemi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE