Afisa mmoja wa polisi wa kike kutoka kituo cha polisi cha Busia amelazimika kuanzisha biashara ya kuuza samaki mjini humo kutokana na kile anadai kuhangaishwa na maafisa wakuu katika idara ya polisi Busia na Kakamega.

Doris Wako ambaye ni mjane na ambaye ameagaziwa na vyombo vya habari kutokana na juhudi zake za kutetea maslahi ya watoto wa kurandaranda (Chokora) amesema amechukua hatua hiyo pamoja na kujiuzulu kazi ya polisi kutokana na kuhangaishwa na idara hiyo.

Anasema masaibu yake katika idara hiyo ilianza pale alipoangaziwa na vyombo vya habari akiwa katika juhudi zake za kuwalea chokora, na hata kupewa tuzo na Rais Kenyatta, ambapo idara hiyo ilianza kumpa uhamisho wa lazima.

Kwa sasa anamtaka KNSpekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai kuitikia kujiuzulu kwake kazini ili aanze maisha mapya ya kulea watoto wake pamoja na kubadilisha maisha ya watoto wa kurandaranda mitaani chokora.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE