Wakazi wa kijiji cha Baharini kinachopakana na Bwawa la Magemo Wadi ya Ndivisi katika eneo bunge laWebuye Mashariki wanaishi kwa hofu baada ya bwawa hilo kufurika maji hali inayohatarisha maisha yao.
Linet Simiyu mmoja wa wakazi eneo hilo, amesema ipo haja juhudi za haraka kuchukuliwa ikiwemo kujenga daraja kurahisisha usafiri la sivyo maji hayo yaondolewe kwenye Bwawa hilo.
Kwa mujibu wa Mzee wa mtaa huo Patrick Wandati, kukosekana kivukio eneo hilo kunatatiza usafiri hasa wanafunzi wanaosoma katika shule kwenye ng’ambo ya pili.
Kwa sasa wakazi hao wametoa makataa ya siku saba kwa idara husika kuitikia kilio chao na kuweka kivukio eneo hilo la sivyo watabomoa kuta za Bwawa hilo ili kuyaondoa maji hayo.
By Hillary Karungani