by Imelda Lihavi

Ni afueni kwa wakenya baada ya  Rais Kenyatta kutangaza kufunguliwa kwa awamu kwa maeneo ya kuabudu. Ibada zitafanyika kwa muda usiopungua lisali moja. Hata hivyo watoto walio chini ya miaka kumi na mitatu na watu wenye umri wa miaka 58, wale walio na matatizo mbalimbali ya kiafya hawataruhusiwa kuhudhuria ibada. Vilevile shule za somo la dini na madrasa hazitaruhusiwa kuendelea.

Rais Kenyatta vilevile alielezea kuwa Marufuku ya kuwa nje kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi alfajiri itaendelea kutekelezwa kwa kipindi kingine cha siku thelathini. Marufuku ya kuandaa mikutano ya hadhara vilevile itadumishwa kwa siku nyingine 30 huku hafla mbalimbali mfano wa harusi, matanga na mikusanyiko ya kisiasa.

Washikadau katika Sekta ya Elimu wamepewa hadi kesho kuchapisha kalenda mpya ya masomo itakayozingatiwa.  Rais Kenyatta ameelezea kusikitishwa na ongezeko la dhulma katika jamii kipindi hiki zikiwamo za kifamilia na dhulma dhidi ya watoto. Kutokana na hali hiyo, Rais Kenyatta amekiagiza kituo cha kukabili uhalifu kuvichunguza visa vyote vya dhulma na kuwasilisha ripoti kwa kipindi cha siku 30 zijazo ili wahusika wachukuliwe hatua.

Marufuku ya usafiri ndani na nje ya kaunti za Nairobi, Mombasa na Mandera itakamilika kesho saa kumi alfajiri baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza kusitishwa kwa marufuku hayo. Katika hotuba kwa taifa, Rais Kenyatta hata hivyo amesema amri hiyo itatekelezwa kwa masharti ambapo serikali itatathimi hali kwa kipindi cha siku 21 na endapo maambukizi ya virusi vya korona yataendelea, marufuku nyingine itatolewa. Safari za ndege za humu nchini zitarejelewa kuanzia tarehe 15 Julai hii huku zile za kimataifa zikirejelewa Agosti 1.

wahudumu wa magari ya umma watahitajika kuwa na cheti cha Wizara ya Afya vilevile sekta ya uchukuzi cha kuhakikisha wamezingatia sheria za kudhibiti maambukizi ya virusi vya korona kabla ya kuendelea na safari hadi kwenye kaunti ambazo awali zilikuwa na marufuku ya usafiri.

Rais Kenyatta hata hivyo amesema serikali haitakuwa ya kulaumiwa endapo watu wengi wataamua kusafiri kuelekea mashinani na kuchangia ongezeko la virusi vya korona. Amesema ni jukumu la kila mtu kuzuia maambukizi zaidi na kuilinda familia yake.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE