LUBAO FREQUENCY MODULATION LIMITED

Uniting Communities
  1. Listen to Lubao FM Live 102.2 FM

Live now:

Up next:

AFUENI KWA WANAFUNZI KUTOKA WADI YA BUTALI CHEGULO KAUNTI YA KAKAMEGA KUJIUNGA NA TTI

Huku shughuli za masomo zikiingia juma la pili katika taasisi zote za elimu nchini zaidi ya vijana 40 wamepata fursa ya kujiunga na chuo cha kiufundi cha Shamberere kupitia kwa afisi ya mwakilishi wa wadi ya Butali Chegulo katika eneo bunge la Malava.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwasajili wanafunzi hao mwakilishi wa wadi hiyo  Kevin Mahelo amehoji kuwa kwenye awamu hii ya pili wameweza kuwasajili  zaidi ya  wanafunzi 40  huku akiwapongeza wazazi eneo hilo  kwa kuitikia mwito huo na kuweza  kuwaleta wanao kujiunga na taasisi hiyo.

Kwa upande wao wazazi wakiongozwa na David Shimaka wameonyesha furaha yao kutokana na mpango huo huku  wakimshukuru mwakilishi wadi huyo kwa kazi nzuri anayofanya hasa katika  sekta ya elimu.   

Hata hivyo Mahelo ametumia fursa hiyo kumkosoa rais Uhuru Kenyatta kufuatia matamshi aliyoyatoa hivi maajuzi kwenye hafla ya mzishi kule Mululu kaunti ya Vihiga akisema kuwa ni njia mojawapo ya kueneza siasa za ukabila.

Charles Oduor

Read Previous

Mtoto ameanguka katika ndoo ya Maji na kufariki katika kata ya Butali eneo bunge la Malava

Read Next

GAVANA OPARANYA ATANGAZA KUWAFUTA KAZI WAHUDUMU WA AFYA WALIO MGOMONI KAUNTI YA KAKAMEGA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *