Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Muyundi kata ya Butali eneobunge la Malava baada ya mtoto mwenye umri wa miaka 2 kuanguka katika ndoo ya maji na kufariki kabla hajafikishwa hosipitalini.

Kulingana na mamake mtoto huyo Rabega Wafula amehoji kuwa alimlaza mtoto huyo kisha akaenda kulima ila alipomaliza na kurudi nyumbani alipata mtoto akiwa ameanguka na kuangalisha  kichwa katika ndo iliyokuwa na maji jambo lililopelekea kifo chake.

Aidha wenyeji wa eneo hilo wakiongozwa na kenedy katakata wamesikitikia kisa hicho na kusema kuwa hiyo ndio mara yao ya kwanza kushuhudia kisa cha mtoto kufia ndooni katika njia tatanishi.

Akithibitisha kisa hicho  Naibu Chifu wa eneo hilo Caleb Wadongo amewarai wamama kuwa wangalifu wanapowalea wanao ili kuzuia maafa zaidi .

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE