Gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya, amesema ataongoza kampeni za mgombea wa chama cha ODM katika uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Matungu utakaoandaliwa mwezi wa  machi tarehe  nne mwaka huu

Akizungumza mjini mumias kwenye kikao na wanachama wa ODM kutoka eneo bunge la Matungu, Oparanya aidha ameteua kamati ya watu saba watakaofanya kazi chini yake kufanikisha azma ya chama hicho kushinda  uchaguzi huo mdogo.

Oparanya ambaye pia ni naibu kiongozi wa chama cha ODM alitumia fursa hiyo kutetea hatua ya chama chake kumteua mbunge wa zamani wa Matungu David Were kupeperusha bendera ya chama cha ODM katika eneo la Matungu

Upande wake Were aliyehudhuria kikao hicho ameahidi kuwashirikisha wajumbe hao kwenye kampeni zake ili kuhakikisha kuwa amechukua uongozi huo

Were atamenyana na Peter Oscar Nabulindo wa chama cha ANC, Alex Lanya wa UDA na zaidi ya wagombea huru sita wanaomeza kiti hicho kilichowachwa wazi kufuatia kifo cha aliyekua mbunge wa Matungu Justus Murunga.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE