Mwanamme mwenye umri wa miaka 38 amepatikana ndani ya chumba chake akiwa amefariki huku mwili wake ukiwa na alama ya visu katika kijiji cha teresia eneo bunge la malava kaunti ya kakamega.  

 Kulingana na esther charles ambaye ni mamake mwendazake aliyefahamika kama ndiwa charles amehoji kuwa marehemu alikuwa buheri wa afya kabla ya mwili wake kupatikana ndani ya chumba chake ukiwa na majeraha ya visu.

 Hata hivyo benard injendi ambaye ni nduguye marehemu amehoji kuwa huenda marehemu aliuawa na watu wasiojulikana na kisha mwili wake kusafirishwa hadi chumbani mwake.

 Naibu chifu wa kata ndogo ya teresia isaac musukuni amethibitisha kisa hicho akiwataka wenyeji kuwa watulivu uchunguzi ukianzishwa huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa kwenye chumba cha wafu cha hospitali kuu ya kaunti ya kakamega ili kufanyiwa upasuaji.


By Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE