Ajuza wa miaka sabini na miwili kutoka kijiji cha Isabane wadi ya Idakho Mashariki eneo Bunge la Ikolomani anaitaka serikali na wahisani kujitokeza na kumjengea nyumba baada ya nyumba yake kuanguka
Sulumena Achitsa ambaye ni mjane anasema kwa sasa amepewa makao na jirani yake lakini kwa sasa jirani anataka nafasi yake
Anasema ako na watoto wawili ambao hawana mapato na hata mvulana wake ametoweka nyumbani hajulikani aliko
By Imelda Lihavi