Maafisa wa polisi eneo bunge la Ikolomani wanamzuilia mwanamme wa miaka 57 kwa jina Polycap Moseti kwa tuhma za kuhusika kwenye kifo cha mwanawe wa kambo wa miaka 11 yapata siku chache zilizopita katika kijiji cha Imalaba.

OCPD wa Ikolomani Joseph Chesire anahoji kuwa mshukiwa akiwa na wengine wawili wanadaiwa kumbaka na kumlawiti  kabla ya kumuua na kisha kutupa mwili wake ndani ya choo ya jirani yake.

Aidha wananchi waliojawa na hamaki walivamia boma na biashara ya mshukiwa na hata kuharibu mimea, nyumba ya biashara kama njia moja ya kutimiza mila desturi ya jamii hiyo.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE