Kundi la akina mama wa chama cha ANC kutoka wadi sita eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega wanaitaka serikali kutuma pesa za wazee hadi mashinani kupitia kwa machifu na  manaibu wao pamoja na watawala wa jamii kuliko kuwaelekeza kuenda kuzipokea kwenye benki wakitumia pesa mingi kusafiri na hata kukosa pesa hizo.

Wakizungumuza baada ya kumtembelea mwanachama wao ambaye anaishi na changamoto ya ulemavu wa mguu na mkono kwa kumpa malazi na chakula  Consolata Kadoko akina mama hao wakiongozwa na mwenyekiti wa eneo la Lurambi Ruth Ombayo wamesikitikia idadi kubwa ya walemavu hao kuteseka kwani  mara si moja wamekuwa wakitumia pikipiki kwa kulipia nauli ili kusafirishwa kutoka vijijini  na wanapofika kwenye baadhi ya benki mjini Kakamega wamekuwa wakikosa pesa hizo.

 Akina mama hao aidha wanasema wameweka siasa kando na kuanza kuwatembelea watu wanaoishi kwa hali duni haswa walemavu,wajane na wengine ambao wako na matatizo mbalimbali wakati huu wa kororna kuona kuwa wanasaidika huku wakilenga zaidi ya akina  walemavu mia tano kutoka wadi sita eneo hilo.

 Wakati uo huo akina mama hao wamewataka machifu kwa ushirikiano nao pamoja na mafisa wa polisi kuwatafuta wanaume ambao wanawabaka akina mama walemavu na watoto ili iwe funzo kwa wengine.

By Boaz Shitemi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE