Zaidi ya wamiliki mia tano wa ardhi katika kaunti ya Kakamega wako katika hatari ya kupoteza umiliki wa ardhi zao kwa kushindwa kuafikia viwango vya manispaa, hii ikiwa ni juhudi za kuimarisha miundo mbinu mjini Kakamega katika mchakato wa kufikia viwango vya jiji mwaka ujao.
Haya yamewekwa bayana na waziri wa ardhi na mpangilio wa mji wa kaunti ya Kakamega, Rorbert Kundu Makhanu, katika mkutano na wamiliki wa ardhi kwenye mtaa huo wa juaka
Makhanu ametumia fursa hiyo kuonya vikali baadhi ya wamiliki ambao wameamua kuuza ploti hizo baada ya serikali ya kaunti kutangaza kuzitwaa tena ploti zote ambazo hazijajengwa akisistiza kuwa sharti sheria za ardhi kutumika
Hata hivyo Makhanu ameeleza kuwa lengo la kuwa na shughuli hiyo nzima si kuwapokonya ardhi wamiliki bali kuhakikisha ardhi zilizopo katikati mwa mji inatumika ipasavyo ili kuinua sura na hadhi ya mji wa Kakamega.